Sakata la Urusi kuingilia uchaguzi Marekani lashika sura mpya, Mwanasheria Mkuu agoma kuhudhuria kikao cha bunge, kisa ripoti ya uchunguzi

  • Next Post
  • Previous Post
default_image_01
Sakata la Urusi kuingilia uchaguzi Marekani lashika sura mpya, Mwanasheria Mkuu agoma kuhudhuria kikao cha bunge, kisa ripoti ya uchunguzi

Kwa mujibu wa shirika la habari nchini Ujerumani la Deutsche WelleUamuzi wa Barr uliotakana na tofauti kuhusu maswali alioulizwa na kamati hiyo, umetokea wakati ambapo wizara yake imeshindwa kutekeleza agizo la kuwasilisha ripoti kamili ya uchunguzi wa Mueller kuhusu madai ya uingiliaji wa Urusi katika uchaguzi pamoja na ushahidi wake.

Hatua hizo zinaweza kusabaisha kura ya kumuwajibisha Barr kwa kudharau bunge, na yumkini kutolewa hati za kuitwa mahakamani jambo linaloweza kusababisha mapambano ya muda mrefu mahakamani kati ya Wademocrat na utawala wa rais Donald Trump.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa na wizara ya sheria, mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya sheria, Jerrold Nadler aliweka masharti mapya kabisa na yasiyokuwa ya lazima kwa waziri Barr.

Hata hivyo, mwenyekiti huyo wa kamati ya sheria amesema ataendelea na kikao cha leo, na kuweka uwezekano wa kuwa na kiti kitupu cha shahidi.

/ Uncategorized

Share the Post

Comments

No comment yet.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

  • Next Post
  • Previous Post
WeCreativez WhatsApp Support
Our customer support team is here to answer your questions. Ask us anything!
👋 Hi, how can I help?